Michezo

Msuva, Mohamed Hussein wang’aa tuzo za Ligi kuu Tanzania Bara “VPL”  2017 (Video + Pic)

Tuzo za Ligi kuu soka Tanzania Bara maarufu kama VPL, zimetolewa Jumatano hii, hafla hiyo ya kukabidhi tuzo mbalimbali za washindi kwa msimu wa mwaka 2016/2017 zimefanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na mgeni rasmi, Dk Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Tamaduni, Sanaa na Michezo.

Dk Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari,Tamaduni,Sanaa na Michezo {katikakati} akiwa katika hafla ya ugawaji tuzo.

 

Simon Msuva, akikabidhiwa tuzo ya Mfungaji bora wa mwaka

“Kitu cha kwanza namshukuru Mungu kwa hii tuzo niliyoipata kwasababu ni kitu ambacho nimejituma kwa uwezo wangu wote. Kingine kuna tuzo ambazo nilitarajia nizipate lakini nimezikosa ni kutokana na vigezo vilivyotumika na TFF pamoja na kamati yao. Kwahiyo mimi nimepokea kwa mikono miwili namshukuru Mungu”.

Mchezaji wa Timu ya Simba SC, Mohamed Hussein mchezaji bora wa mwaka.

Mohammed Hussein Mchezaji bora wa mwaka 

“Kwa kweli najisikia vizuri sana na nimejisikia faraja kuona mwanangu amepata tuzo ya mchezaji bora kwa mwaka huu. Nawaambia wazazi wenzangu ambao watoto wetu wanacheza mpira, tusione kama mpira ni uhuni tuzidi kuwasaidia watoto,” alisema mzazi wa Mohamed Hussein.

Mchezaji wa Timu ya Yanga SC, Haruna Niyonzima akipokea tuzo yake

 Haruna Niyonzima, mchezaji bora wa kigeni wa Mwaka

Mchezaji wa Timu ya Yanga SC, Haruna Niyonzima alisema “Naamini hata kama nimechaguliwa kuwa mchezaji bora wa kigeni sio kwamba mimi nimewazidi wenzangu”.

 

Mchezaji wa timu ya Kagera Sugar, Mbaraka Yusuph,

Mbaraka Yusuph , Mchezaji bora anae chipukia 
Mbaraka Yusuph,Mchezaji wa Kagera Sugar, “Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupata tuzo hii”.

Mchezaji wa Timu ya Azam FC, Aishi Manula, akipokea tuzo

Aishi Manula, Goikipa bora wa Msimu

 

Mchezaji wa Timu ya JKT Ruvu,  Abdulrahman Mussa akipokea tuzo

Abdulrahman Mussa,  Mfungaji bora wa mwaka huyu na Simon Msuva wana lingana magoli wote wana magoli 14

Muamuzi wa Ligi kuu , Elly Sasii, akipokea tuzo

Elly Sasii, amechagukiwa kuwa Mwamuzi bora wa mwaka.

 

Klabu ya Yanga ikipokea hundi yenye thamani ya Shili Milioni themani na Nnen ikiwa ni klabu a kwanza, hundi hiyo inapokelewa naCharles Boniface Mkwasa 

Klabu ya Simba SC, ikipokea hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni arobaini na mbili

Kikosi bora cha TFF, cha mwaka, ikiwa ni mjumuisho ya wachezaji 11 kutoka katika timu tofauti

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents