Habari

Mtalii afariki kwenye maji akimchumbia mpenzi wake wakiwa Tanzania- Video

Mtalii afariki kwenye maji akimchumbia mpenzi wake Tanzania- Video

Mtalii mmoja amekufa maji baada ya kumchumbia mchumba wake chini ya maji nchini Tanzania wakati wa likizo.

Kulingana na mtandao wa Sky News, Steven Weber na Kenesha Antoine walikuwa wakiishi katika hoteli moja ya mbao ambayo ipo chini ya maji nchini humo ili kuwawezesha kuona kilichopo majini

Picha zimeonyesha wakati bwana Weber kutoka eneo la Baton Rounge mjini Luoisiana Marekani, alivyoogelea hadi katika dirisha moja lililopo chini ya maji kabla ya kushika karatasi akimuomba bi Antoine kufunga naye ndoa.

Karatasi hiyo ilisoma: Siwezi kuzuia pumzi zangu kwa muda mrefu ili kukwambia kila kitu ninachokupendea lakini kila kitu ninachokupendea nakupendea kila siku.

Bwana Weber baadaye aliibadilisha karatasi hiyo ili kuonyesha maneno aliyokuwa ameandika upande mwengine yaliosema: Je tafadhali unaweza kuwa mke wangu? Utafunga ndoa nami???.

Kulingana na mtandao wa Sky News, baadaye alitoa pete ya uchumba kutoka katika mfuko wake kabla ya kuogelea na kuondoka eneo hilo.

Bi Antoine naye alichapisha picha za kisa hicho katika facebook ambapo anaonekana akifurahia pamoja na tamko lake: Ndio! Ndio! Ndio!.

Lakini mrembo huyo baadaye alichapisha habari mbaya kwamba mpenzi wake alifariki.

Bi Antoine alisema kwamba hakurudi akiwa mzima baada ya kuogelea baharini.

Wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani ilisema kwamba mtalii mmoja wa Marekani amefariki nchini Tanzania lakini hakuna maelezo zaidi yalioripotiwa.

Hoteli ya chini ya maji Pemba

Bi Antoine aliandika: Hakuna maneno yatakayotoa heshima kwa mpenzi wangu Steven Weber jr.

“Hukutokezea tena kutoka kina hicho cha bahari hivyobasi hukuweza kusikia nikikubali mara milioni kwamba ndio nitafunga ndoa nawe”!

”Hakutuweza kukumbatiana na kushrehekea mwanzo wa maisha yetu yaliosalia, baada ya siku bora zaidi katika maisha yetu kuwa mbaya Zaidi”.

”Nitajaribu kujifariji kwa kuwa tulifurahia siku zetu za hivi karibuni na kwamba sote tulikuwa tumejawa na furaha wakati wetu wa mwisho”.

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents