Habari

Mtandao dawa za kulevya watinga magerezani

Jeshi la Magereza limetakiwa kutafuta mbinu za kisasa za kuwakamata watu walioko magerezani ambao wanaendeleza mawasiliano na mitandao ya uhalifu iliyoko uraiani na hasa katika dawa za kulevya na ujambazi.

Akifungua mkutano wa maofisa waandamizi wa jeshi hilo katika mkutano wa mwaka uliofanyika Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisema kwa taarifa aliz nazo ni kwamba baadhi ya wahalifu wanaendeleza mawasiliano na wenzao walio nje.

“Nimefanya utafiti wangu kuna mtu nilimtuma huko ndani na nimebaini kuna watu waliopo gerezani bado wanaoperate na mitandao yao ya uhalifu kama magenge ya dawa za kulevya,” alisema Mwigulu. Alilitaka Jeshi hilo kutafuta mbinu za kisasa za kuwakamata watu hao pamoja na mitandao yao iliyoko uraiani.

“Endapo tutawakamata watuhumiwa au wafungwa hao ambao bado wanaendeleza mawasiliano, tumieni mwanya huo kuukamata mtandao mzima wanaofanya nao mawasiliano kwa kutumia simu zao washitakiwe,” alisisitiza.

Alisema anafahamu kwamba askari magereza wanajitahidi kupambana na wahalifu hao walioko magerezani na kuwataka kuongeza jitihada hizo. Aidha akizungumzia mbinu za kisasa, alisema ni pamoja na kufunga mtambo maalumu utakaowezesha kukata mawasiliano yoyote ya mitandao ya simu katika eneo la magereza ili kusiwe na mawasiliano hayo.

Na Emmy Mwaipopo

Chanzo: Habarileo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents