Habari

Mtandao wa biashara ya ngono wavunjwa

By  | 

Polisi nchini Uhispania imewaokoa wanawake 13 waliokuwa wakifanya kazi ya ukahaba na uporaji watu katika mji wa Puerto Banus.

Wanawake hao ambao kwa sasa wapo huru waliletwa katika eneo hilo, wakitokea nchini Bulgaria, na walifika hapo wakalazimishwa kufanya kazi za ukahaba katika kituo kimoja cha utalii.

Inaelezwa kuwa wanawake hao walilazimishwa pia kufanya biashara ya uporaji mali mtaani na kutumia madawa ya kulevya. Kukamatwa kwa watu hao, kumekuja takribani miaka mitatu baada ya polisi kujulishwa kuhusu mtandao huo.

Polisi wamefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa 34 ambao walikuwa wakihusika na mtando huo katika nchi zote mbili, pia wamekamata mali zao kama vile magari na kuzifungia akaunti zao za kibenki ilikufanya uchunguzi.

Na Laila Sued

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments