Technology

Mtandao wa Facebook umeunda mfumo huu mpya, unaolenga kubaini watu wanaoweka matangazo ya uongo kwenye mtandao huo

Facebook imeunda mfumo huu mpya unaowalenga kubaini watu wanaoweka matangazo ya uongo kwenye mtandao huo

Facebook imeunda mfumo mpya unaowalenga watu wanaoweka matangazo ya uongo kwenye mtandao huo. Mfumo huo umekuja baada ya Martin Lewis, mwanzilishi wa tovuti ya Money Saving Expert, kushtakiwa baada ya jina na picha yake kutumika kwenye matangazo bandia kwenye ukurasa wa Facebook.

Kwa mujibu wa bbc. Facebook iliamua kuchangia kiasi cha pauni milioni 3 kwa ajili ya kutengeneza programu ya kupambana na wadanganyifu nchini Uingereza.

Taasisi ya kujitolea ya Citizens Advice imebuni laini ya simu ili iweze kuwasaidia watu wanapokutana na wadanganyigu mitandaoni-si tu kwa matangazo.

Kadiri siku zinavyosonga mbele vitendo vya kitapeli vinazidi kuongezeka, hivyo taasisi hiyo inatarajia kuwasaidia watu 20,000 mwaka wa kwanza wa huduma watakayoitoa, na kutahadharisha kuwa mtu yeyote anaweza kuingia kwenye mtego huu.

Citizens Advice imeainisha viashiria vitakavyojulisha kuwa matangazo ni bandia

  • Tangazo lisilo na uhalisia-au bidhaa iliyo na gharama ya chini kuliko inavyotarajiwa.
  • unapoambiwa ulipe haraka sana, au kwa njia isiyo ya kawaida-labda kwa huduma za kuhamisha fedha au kwa kutumia vocha.
  • Mtu kuwasiliana na wewe bila kutarajia.
  • kuulizwa kuhusu taarifa zako binafsi kama vile nywila (password) au pini.
  • tangazo lenye picha za watu maarufu .

Ndani ya Facebook, timu ya watu wenye ujuzi imeundwa kwa ajili ya kuchunguza matangazo yaliyoripotiwa kwa kutumia mfumo huu mpya.

Kuanzia siku ya Jumanne, Watumiaji wa Facebook nchini Uingereza wataweza kubofya sehemu yenye madoa matatu kwenye ukingo wa kila tangazo, ili kuweza kuripoti matangazo yaliyo ya udanganyifu.

Hali ikoje?

Miaka michache baada ya mume wake kufariki, Amanda- si jina halisi-aliingia kwenye mtandao wa kutafuta wapenzi akitafuta rafiki.

Baada ya muda, alianza kuwasialiana kwa email na mtu mmoja ambaye alikuwa akimfurahia. Wiki chache baadae, ”aliuliza kama Amanda anaweza kumtumia pesa”, alieleza.

”Hakuwa amelipwa na alihitaji kusafiri kurudi nyumbani akitokea Ireland. Sikufikiri sana na nikamtumia fedha.”

Wawili hao waliendelea kuudumisha urafiki wao kwa miezi kadhaa- kisha akaomba tena pesa kwa nyakati tofauti tofauti.

Lakini kwa Amanda akaona kuna kitu hakipo sawa- kisha akaamua kutomtumia ujumbe tena.

Baada ya majuma machache kupita Amanda alipata ujumbe kutoka kwenye tovuti ya wapenzi- ikiwa na picha ileile, lakini kwa jina tofauti na eneo tofauti.

”Hapo ndipo nilipobaini kuwa pengine nilikuwa nikizungumza na mtu ambaye si mwenye picha,” Amanda alieleza.

Kwa kipindi cha miezi kadhaa, alikuwa ametuma kiasi cha pauni 2,500 kwa watu waliokuwa wakiwasiliana naye.

”Ninafikiri labda baadhi ya wanaume hujiunga kwa wingi kwenye tovuti kwa kuwa wanajua kuwa kuna wanawake kama mimi ambao wanataka urafiki ili kuweza kujinufaisha

MatangazoHaki miliki ya pichaMONEYSAVINGEXPERT

Mamilioni ya watu wanajua kubaini matangazo bandia wakiyaona. Na mamilioni hawajui, hivyo wataalamu wanashauri kuyatambua kwa kutumia mfumo mpya wa kuripoti kwenye Facebook, na kuwalinda wale wasiojua.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents