Tia Kitu. Pata Vituuz!

Mtandao wa Facebook umezindua utaratibu huu maalumu wa kuanza kuwalipa watumiaji wake

Mtandao wa Facebook umezindua utaratibu huu maalumu wa kuanza kuwalipa watumiaji wake

Mtandao wa Facebook umeweka utaratibu wa kuwalipa watumiaji wake kwa kusoma kurasa za maandishi kwa sauti, ili kuimarisha mfumo wake wa utambuzi wa sauti.

Mtandao wa Facebook

Utaratibu huo unafanywa kupitia ‘app’ yake mpya ya utafiti wa maoni ya masoko (market research app Viewpoints), ambapo utatumika kufundishia mfumo wa utambuzi kwenye mfumo mkuu wa taarifa za Facebook.

App hiyo ya maoni katika mitandao ya kijamii ilizinduliwa miezi mitatu iliyopita kwa ajili ya kujaribu viungo vipya (features), ambapo wiki iliyopita ilianza kuwaalika watumiaji wa Facebook nchini Marekani kwa ujumbe unaosema “Hey Portal” pamoja na majina ya rafiki wa mtumiaji wapatao 10.

Zoezi hilo linachukua dakika tano likiwa na jumla ya pointi 1000 ambapo ukikamilisha unalipwa Dola 5 (Sh.11521) na pesa hiyo itatumwa moja kwa moja kwa mhusika kupitia njia ya mtandao (Pay pal).

Mtumiaji atarekodi takribani mara tano, ambapo mara moja inampa pointi 200 na kwa mara tano inampa pointi 1000 ambazo ni sawa na Dola 5 (Sh.11521).

Utaratibu huo hutumika na makampuni mengine makubwa ya kibiashara kama Amazon, Apple na Google lakini umeleta sintofahamu kwa jinsi wanavyokusanya na kuzipitia sauti za watumiaji. Makampuni hayo hutumia utaratibu wa makubaliano ya siri ambapo watumiaji wengi hukubali bila kujua matokeo yake.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW