Fahamu

Mtandao wa Facebook waeleza kufuta mamia ya akaunti fake katika mataifa haya 5 ya Afrika kati ya 6 bado taifa hili

Mtandao wa Facebook waeleza kufuta mamia ya akaunti fake katika mataifa haya 5 ya Afrika kati ya 6 bado taifa hili

Facebook imeondosha mamia ya akaunti za mitandao ya kijamii na kupiga marufuku kampuni ya Israel kutokana na inachotaja kuwa “Tabia za uongoz zilizoratibiwa” zinazoilenga Afrika. Akaunti hizo bandia mara nyingi huweka taarifa za kisiasa, ikiwemo uchaguzi katika baadhi ya mataifa , kampuni hiyo imesema.

Kwa mujibu wa BBC. Facebook imekabiliwa na shutuma kwa kushindwa kudhibiti taarifa za uongo katika jukwaa hilo la mtandao wa kijamii.

Ilizindua mradi wa kuangalia uhakika wa taarifa mnamo 2016 muda mfupi baadaya rais Trump wa Marekani kuingia madarakani .

Katika ujumbe kwenye blogu, Facebook imesema imeondosha akaunti 265 za mtandao wa kijamii zilizofunguliwa nchini Israel na zilizoilenga Nigeria, Senegal, Togo, Angola, Niger na Tunisia, pamoja na kushuhudiwa “sehemu ya shughuli zake” Amerika kusini na Kuisni mashariki mwa Asia.

“Watu wanaohusika na mtandao huuwalitumia akaunti bandia kuendehsa kurasa hizo, kusabaza taarifa zao na kuongeza mawasiliano kwa njia za uongo.

“Walijifanya kuwa watu kutoka mataifa hayo, wakiwemo kutoka vyombo vya habari nchini, na kuchapisha na kutuhumiwa kufichua taarifa kuhusu wanasiasa” Nathaniel Gleicher, mkuu a kitengo cha kupambana uhalifu wa mtandaoni katika Facebook, ameandika katika ujumbe huo.

Uchunguzi umebaini kwamba shughuli hizo zimehusishwa na kampuni ya Israeli – Archimedes Group, Gleicher ameongeza.

“Shirika hilo na matawai yake sasa yamepigwa marufuku kutoka Facebook, na kupewa onyo kali la kusitisha shughuli hizo,” amesema.

Wahusika wa akaunti hizo walitumia $812,000 kwa matangazo kati ya Disemba 2012 na April 2019, Facebook imesema, na fedha hizo zimelipwa kwa kutumia sarafu ya Brazilian reais, ya Israeli shekel na dola za Marekani.

Nchi tano kat iya 6 za Afrika zilizolengwa zimekuwana uchaguzi tangu 2016 na Tunisia itaanda uchaguzi baadaye mwaka huu.

Facebook imeshutumia kwa kushindwa kukabiliana na habari ghushi ambazo zinaweza kuathiri namna watu wanavyopiga kura katika uchaguzi.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents