Technology

Mtandao wa Facebook waendeleza msako wa kuzifutilia mbali akaunti fake, waeleza sababu za kufuta zaidi ya akaunti bilioni 3

Mtandao wa Facebook waendeleza msako wa kuzifutilia mbali akaunti fake, waeleza sababu za kufuta zaidi ya akaunti bilioni 3

Mtandao wa Facebook umechapisha orodha ya mabilioni ya akaunti feki ilizochukulia hatua kati ya mwezi Oktoba 2018 na Machi 2019. Katika kipindi hicho cha miezi sita, Facebook ilifunga zaidi ya akaunti bilioni tatu feki – idadi ambayo inasema ni kubwa zaidi kuwahi kufungwa.

Zaidi ya ujumbe milioni saba za”chuki” pia zilitolewa katika mtandao huo wa kijami.

Kwa mara ya kwanza, Facebook pia iliripoti kuwa baadhi ya watumiaji wa mtandao huo ambao ujumbe wao ulifutwa wamekata rufaa na kuongeza kuwa zingine zilirudishwa baada ya uchunguzi wa kina.

Kwa mujibu wa BBC. Akizungumza na vyombo vya habari mwanzilishi wa mtandao huo Mark Zuckerberg aliwakosoa vikali wale ambao wanatoa wito kampuni hiyo ivunjiliwe mbali, akiongeza kuwa wanafanya kila wawezalo kukabiliana na changamoto zinazoibuka.

Mtumiaji wa facebook kwa simuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

“Sidhani suluhisho ni kuvunjilia mbali kampuni kwasababu tunashughulikia [tatizo hilo],” alisema.

“Ufanisi wa kampuni hii umetuwezesha kufadhili mpango huu kwa kiwango kikubwa. Kiwango cha fedha tunazotumia kuimarisha usalama wa mtandao wetu ni kikubwa kuliko ”mapato ya mwaka mzima” ya mtandao wa Twiter.

Akaunti Bandia

Facebook imesema kumekuwa na ongezeko la akaunti bandia kwasababu “wahalifu” wamekuwa wakitumia mfumo maalum kuzifungua.

Lakini ikaongeza kuwa ilifanikiwa kuzigundua na kuzifuta zote katika kipindi cha dakika moja, kabla wapate nafasi ya kuzitumia kufanya “uhalifu “.

Mtando huo wa kijamii pia utaripoti ni posti zilizotolewa kwa kuuza “bidhaa ambazo zimedhibitiwa”kama vile bunduki na dawa.

Facebook logoHaki miliki ya pichaREUTERS

Ilisema kuwa iliwachukilia hatua watumiaji milioni moja wa mtandao huo kwa kuuza bunduki katika miezi hiyo sita kipindi ambacho ilichukua kuaanda ripoti hiyo.

Ripoti hiyo pia ilikadiria idadi ya ujumbe, kama zile zinazoangazia unyanyasaji watoto, ghasia na propaganda kuhusu ugaidii,zinazowafikia wateja wake.

Uchunguzi huo ulibaini ni mara ngapi posti 10,000 zilizo na ujumbe huo zilionekana kwenye Facebook:

  • Watu wachache kati 14 waliona picha za utupu
  • Karibu watu 25 waliona taarifa zilizo na ujumbe wa kuchochea ghasia
  • Wachache kati ya watu watatu waliona taarifa zilizo na ujumbe wa unyanyasaji wa watoto na propaganda kuhusu masuala ya ugaidi

Kwa ujumla, karibu ya 5% ya watumiaji wa mtandao huo wanafanya hivyo kupitia akaunti feki.

Rufaa

Kwa mara ya kwanza, ripoti hiyo ilifichua kuwa kati ya mwezi Januari na Machi 2019 zaidi ya watumiaji milioni moja wa mtandao huo walikata rufaa baada ya akaunti zao kufungiwa kwa kuposti ujumbe uliyo na ”kauli za chuki”.

Karibu watumiaji 150,000 walifunguliwa akaunti zao baada ya kubainika kuwa hawakukiuka sheria kipindi hicho.

Facebook imesema ripoti hiyo imeangazia masuala hayo ili kuendesha huduma zake kwa njia ya uwazi na uwajibikaji ili kuufanya mtandao huo kuwa ”salama kwa wateja wake”.

Hivi karibuni Facebook iliondosha mamia ya akaunti za mitandao ya kijamii na kupiga marufuku kampuni ya Israel kutokana na inachotaja kuwa “Tabia za uongoz zilizoratibiwa” zinazoilenga Afrika.

Akaunti hizo bandia mara nyingi huweka taarifa za kisiasa, ikiwemo uchaguzi katika baadhi ya mataifa , kampuni hiyo imesema

Facebook imekabiliwa na shutuma kwa kushindwa kudhibiti taarifa za uongo katika jukwaa hilo la mtandao wa kijamii.

Kampuni hiyo ilizindua mradi wa kuangalia uhakika wa taarifa mnamo 2016 muda mfupi baadaya rais Trump wa Marekani kuingia madarakani .

Katika ujumbe kwenye blogu, Facebook ilisema imeondosha akaunti 265 za mtandao wa kijamii zilizofunguliwa nchini Israel na zilizoilenga Nigeria, Senegal, Togo, Angola, Niger na Tunisia, pamoja na kushuhudiwa “sehemu ya shughuli zake” Amerika kusini na Kuisni mashariki mwa Asia.

Walikuwa na majina kama ‘Hidden Africa’ na siri ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Ujumbe huo ulionekana kumuunga mkono rais mpya wa Felix Tshisekedi na kumuomba mgombea wa upinzani akubali kushindwa.

Facebook logoHaki miliki ya pichaREUTERS

“Watu wanaohusika na mtandao huu walitumia akaunti bandia kuendesha kurasa hizo, kusambaza taarifa zao na kuongeza mawasiliano kwa njia za uongo.

“Walijifanya kuwa watu kutoka mataifa hayo, wakiwemo kutoka vyombo vya habari nchini, na kuchapisha na kutuhumiwa kufichua taarifa kuhusu wanasiasa” Nathaniel Gleicher, mkuu a kitengo cha kupambana uhalifu wa mtandaoni katika Facebook, ameandika katika ujumbe huo.

Uchunguzi huo ulibaini kwamba shughuli hizo zimehusishwa na kampuni ya Israeli – Archimedes Group, Gleicher ameongeza.

“Shirika hilo na matawi yake sasa yalipigwa marufuku kutoka Facebook, na kupewa onyo kali la kusitisha shughuli hizo,” alisema.

Wahusika wa akaunti hizo walitumia $812,000 kwa matangazo kati ya Disemba 2012 na April 2019, Facebook imesema, na fedha hizo zimelipwa kwa kutumia sarafu ya Brazilian reais, ya Israeli shekel na dola za Marekani.

By Ally Juma.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents