Aisee DSTV!

Mtandao wa Google wamuenzi mwandishi maarufu wa fasihi, Margaret Atieno Ogola kutoka Kenya, Mfahamu kiundani mwandishi huyu

Mtandao wa Google wamuenzi mwandishi maarufu wa fasihi, Margaret Atieno Ogola kutoka Kenya, Mfahamu kiundani mwandishi huyu

Kumekuwa na msisimko mkubwa miongoni mwa Wakenya katika mitandao ya kijamii kufuatia hatua ya Google kumuenzi mwandishi maarufu wa fasihi nchini humo. Margaret Atieno Ogola amekumbukwa leo, siku ambayo angelikuwa hai angekuwa anatimiza miaka 60 tangu kuzaliwa kwake.

Kwa mujibu wa BBC. Alipata umaarufu mkubwa kwa kitabu chake cha kwanza kilichosomwa na wengi nchini, ‘The River and the Source’, ambacho kilijishindia tuzo ya fasihi ya Jomo Kenyatta mnamo 1995 na pia zawadi kwa kitabu cha kwanza bora ya tuzo ya waandishi wa Jumuiya ya madola.

Kitabu hicho kilichotumika katika mtaala wa shule za upili katika miaka ya 90 kinaangazia maisha ya vizazi tofuati vya wanawake nchini Kenya tangu vijijini mpaka katika maisha ya kileo mjini Nairobi.

Kitabu hicho kilichotumika katika mtaala wa shule za upili katika miaka ya 90 kinaangazia maisha ya vizazi tofuati vya wanawake nchini Kenya tangu vijijini mpaka katika maisha ya kileo mjini Nairobi.

Kwa jumla, ‘The River and the Source’ kimegusia uwezo wa wanawake wa Kiafrika katik maisha yao ya kila siku.

Baadhi ya mashabiki wa mwandishi huyo maarufu waliopata fursa ya kusoma baadhi ya vitabu vyake wamenuku baadhi ya dondoo kutoka vitabu hivyo katika ujumbe wa kumuenzi na kufurahia hatua ya Google leo kumkumbuka Margaret.

Mwandishi huyo amesifiwa kwa kuiweka fasihi ya Kenya katika ramani ya dunia:

Margaret Atieno Ogola ni nani?

Katika nakala ya kumbukumbu alioandika mwandishi wa Kenya Joseph Adero Ngala, amesema ‘Haishangazi kuwa Ogola anasikika kwa uwazi katika sauti za wanaomkumbuka leo’.

Ogola aliandika vitu vinavyohusu duniani. Katika uandishi wake alibadili mtazamo na mtindo wake kulingana na changamoto zinazomkabili mithili ya msanii maarufu Picasso, anaeleza Ngala. Margaret Ogola alikuwa mwandishi, Daktari wa watoto ma mkereketwa wa kutetea haki za binaadamu.

Alizaliwa mnamo Juni 12 mwaka 1958 na alisoma katika mojawapo wa shule bora za wasichana Nairobi, Alliance Girls High School.

Baada ya hapo alijiunga katika chuo kikuu cha Nairobi na kupata shahada, katika masuala ya uapsuaji na dawa mnamo 1984.

Baada ya kuhitimu chuo kikuu alifanya kazi kama afisa wa afya katika hospitali ya kitiafa ya Kenyatta.

Yeye ni mama wa watoto wanne. Kwa waliomfahamu kwa karibu, wanasema Margaret alikuwana maoni makali lakini mtazamo wa kadri. Alipenda kuwasikiliza watu. Wengine wanamfahamu kwa ukarimu na ucheshi wake. Aliugua na kufariki kutokana na ugonjwa wa saratani mnamo Septemba 12, mwaka 2011.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW