Michezo

Mtandao wa Halotel kushirikiana na SportPesa watangaza habari njema kwa Watanzania (+Video)

Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi Tanzania ya Halotel leo Novemba 28, 2017 imeingia makubaliano rasmi na Kampuni ya kubashiri michezo ya SportPesa ili kuongeza msisimko na ushirikiano kwa wadau wa michezo ya kubashiri nchini.

Maafisa Habari wa SportPesa na Halotel wakikabidhiana mikataba.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Halotel, Mhina Semwenda akiongea mbele ya Waandishi wa Habari leo katika Ofisi za Makao Makuu ya Mtandao huo amesema ushirikiano huo utawawezesha watumiaji wa Halotel kupitia huduma ya kifedha ya HaloPesa kupata nafasi ya kubashiri michezo mbalimbali na SportPesa kama inavyofanya mitandao mingine ya simu.

Ushirikiano wetu na SportPesa utawawezesha wateja wetu kuweza kufurahia kushiriki katika michezo mbalimbali ya kubashiri kwa urahisi, kupitia huduma zetu za kifedha za HaloPesa,“amesema Semwenda huku akielezea wigo wa masafa ya mtandao huo.

Mtandao wetu umeenea zaidi katika maeneo ya vijijini, jambo ambalo sasa linatoa fursa mpya ya ushiriki katika michezo ya kubashiri kwa wateja wetu ambao awali walikuwa hawapati fursa hiyo ya kubashiri. Tunaamini kwa sasa zaidi ya vijiji 4000 ambavyo mtandao wetu unapatikana watafurahia huduma hiyo ya kubashiri michezo mbalimbali kutoka SportPesa.“amesema Semwenda.

Mtandao wa Halotel ambao mpaka sasa una mawakala 50,000 nchi nzima wateja wake watafaidi kutabiri michezo ya aina mbalimbali na kujishindia mamilioni ya fedha pamoja na zawadi mbalimbali zikiwemo Bajaj, Jezi na Tiketi za kwenda kushuhudia mechi live nchini Uingereza kupitia promosheni ya Shinda na SportPesa.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa SportPesa, Sabrina Msuya amesema ushirikiano huo ni nafasi nzuri kwa Watanzania na mtandao wa Halotel kwani wamekuwa wakipata maombi mengi kutoka kwa Wateja wao wakitaka kuwezeshwa kushiriki kwenye michezo ya kubashiri.

Hii ni nafasi nzuri kwetu na kwa wateja wa Halotel kwani tulikuwa tunapokea maombi mengi juu ya uhitaji wao wa kushiriki kubashiri na SportPesa kama ilivyo kwa mitandao mingine,“amesema Msuya.

Je, kwa mteja wa Halotel atawezaje kujiunga au Kubeti na SportPesa? Fuata maelekezo yafuatayo.

Mteja wa Halotel unatakiwa kutuma neno GAME kwenda 15888 ili kujisajili, na ili mteja uliyejisajili uanze kucheza (kubet) na SportPesa ongeza kwanza salio kwenye akaunti yako ya SportPesa kwa kupiga namba *150*88#, kisha chagua lipa bili na HaloPesa, kisha chagua 4. Ambapo itakuletea neno Michezo ya Kubahatisha kisha bonyeza 1 ambayo ni SportPesa (150888) kisha ingiza kumbukumbu namba ambayo ni 888, kisha weka namba yako ya siri kumaliza kujisajili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents