Burudani

Mtandao wa Instagram sasa una thamani ya dola bilioni 35!

Uamuzi wa Facebook kuinunua Instagram ulikuwa sawa na kulamba karata dume.

instagram-tilt

Citigroup imedai kuwa imepiga thamani ya Instagram na sasa inaamini kuwa mtandao huo una thamani ya dola bilioni 35.

Awali, Citi iliuthaminisha mtandao huo na kusema una thamani ya dola bilioni 19. Facebook iliinunua Instagram mwaka 2012 kwa thamani ya dola bilioni 1 peke yake.

Kuongezeka kwa thamani hiyo ya Instagram kumetokana na tangazo lake la wiki iliyopita kuwa kwa sasa ina watumiaji zaidi ya milioni 300 kwa mwezi, na hiyo ikimaanisha kuwa unakua haraka kuliko ilivyotarajiwa.

Citigroup inaamini pia kuwa muda si mrefu, Instagram itaweza kuchangia karibu dola bilioni 2 za mapato ya Facebook kwa mwaka kama ikiamua kuutumia kuingiza fedha. Mapato mengi ya Facebook, bado yanayoka kutoka kwenye mtandao wa Facebook wenyewe, lakini Citi inatarajia kuwa Facebook itaanza kuingiza pia fedha kutoka kwenye app zake zingine.

Chanzo: The Verge

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents