Tupo Nawe

Mtandao wa Instagram wabuni njia hii ya kuwakomesha watumiaji wanaotuma ujumbe wa kuzalilishana na kutukanana

Mtandao wa Instagram wabuni njia hii ya kuwakomesha watumiaji wanaotuma ujumbe wa kuzalilishana na kutukanana

Mtandao wa Instagram unaamini kuwa kuwepo kwa ujumbe wa kuwafanya watumiaji wa mtandao kufikiri kuhusu wanachokisema, utasaidia kuondokana na vitendo vya udhalilishaji mtandaoni. Hivi karibuni itawapatia watu wanaodhalilishwa mitandaoni uwezo wa kuzuia majibizano na watumiaji wanaowadhalilisha.

Kwa mujibu wa BBC. Instagram imekuwa kwenye changamoto ya kupambana na tatizo la udhalilishaji baada ya madhara makubwa kutokea kama tukio la kujiua kwa binti mmoja wa nchini Uingereza.

”Tunaweza kufanya zaidi kuepuka vitendo hivi kufanyika kwenye instagram, na tunaweza kuchukua hatua zaidi za kuwawezesha walengwa wa vitendo hivyo ili waweze kujitetea wenyewe”.ameeleza mtendaji mkuu Adam Mosseri.

Facebook imekuwa ikilaumiwa kutodhibiti mitandao yao, sasa wajipanga kuchukua hatua

Fikiri tena

Instagram imesema imekuwa ikitumia teknolojia ya kubaini kama ujumbe unafanana na aina ya ujumbe unaowekwa ambao umekuwa ukiripotiwa kuwa usiofaa kwa watumiaji.

Katika mfano mmoja, mtu ataandika ”wewe ni mbaya na mpumbavu.” kisha ujumbe utamfikia kutoka instagram ukimuuliza: ”Una uhakika unataka kuweka ujumbe huu? fikiri zaidi”.

Ikiwa mtumiaji atabofya palipoandikwa ”fikiri zaidi” ujumbe utatokea ukisema ” tunauliza watu kufikiri kuhusu kauli zinazoonyesha kufanana na zile zinazoripotiwa kuwa mbaya.”

Molly Russell, binti aliyejiua mwaka 2017Haki miliki ya pichaFAMILY HANDOUT/PA WIRE

Mtumiaji anaweza kupuuza ujumbe na kuweka ujumbe wake, lakini Instagram ilisema kwa majaribio ya awali yanaonyesha kuwa wataweza kuwafanya watu kufuta ujumbe mbaya na kuandika kitu kingine kisichomuudhi mtu ikiwa watakuwa na nafasi ya kutafakari.

Uwezo huo unaanzia kwa nchi za watu wanaozungumza kiingereza,kukiwa na mipango ya huduma hiyo kufika duniani kote, Instagram imeiambia BBC.

Mipaka

Kampuni imesema pia itakuja na kifaa kingine, kiitwacho Restrict (zuia),kilichoundwa kusaidia watoto kuchuja maneno bila kuwafungia wanaowadhalilisha hatua ambayo imeripotiwa kuleta matokeo chanya kwa dunia.

”Tumewasikia vijana kwenye jamii yetu kuwa wamekuwa wakishindwa kuwafungia, au kuwaondoa kwenye orodha ya marafiki au kuripoti vitendo vyao vya udhalilishaji wakihofu kuendelea kwa vitendo hivyo, alisema Mosseri.

InstagramHaki miliki ya pichaPA

Ikiwa mtumiaji atazuiwa ujumbe atakaotuma utaonekana kwa mtumaji peke yake, la muhimu ni kuwa mtumaji hatajua kama amezuiwa

Watu waliozuiwa hawatakuwa na uwezo wa kuwaona waliowazuia kama wanapatikana Instagram au wakati unaposoma ujumbe wao wa moja kwa moja.

‘Hakuna sababu ya kujitetea’

Udhalilishaji kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram, ulitazamwa kwa jicho la tatu mwanzoni mwa mwaka huu.

Baba wa binti wa miaka 14 Molly Russell, aliyejiua , amesema vitu vya kufedhehesha alivyokutana navyo kuhusu msongo wa mawazo na kujiua ni sehemu ya sababu za kujiua kwa binti yake.

Mwezi Aprili serikali ya Uingereza ilipendekeza kuwepo kwa sera itakayodhibiti makampuni ya teknolojia. Kuundwa kwa chombo huru kitakachodhibiti namna masuala ya udhallishaji yatakavyoshughulikiwa.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW