Promotion

Mtandao wa Mambopoint kuzinduliwa rasmi Julai, sasa wafikisha users 9,000

Mtandao wa kijamii wa Mambopoint ambao ulikuwa kwenye majaribio toka mwezi Desemba mwaka 2012, unatarajiwa kuzinduliwa rasmi Julai 13 mwaka huu.

mambo-point-500x329

Mkurugenzi Mtendaji wa Maarifa Informatics Limited ambao ndio wamiliki wa mtandao huo, Mahamud Masoud anasema walianza kuutengeneza July 2012 na baadaye mwezi Desemba kuutangaza kwa lengo la kupata watumiaji kidogo ili kupata uzoefu.

Watu walichangamkia na kujisajili ambapo katika siku tatu tu tangu kutangazwa kwake watu 512 walikuwa wamejisajili.

“Hadi sasa tuna watu 9351 na active users mpaka leo 25th June 2013 saa 11:36 ni watu 2765. Watumiaji ni kutoka Africa Mashariki yote, baada ya uzinduzi naamini watumiaji watakuwa wengi zaidi” anasema Masoud.

Lengo la mtandao huu ni kutumia mitandao ya kijamii kuwapatia watu manufaa ya kiuchumi kama nafasi za kazi, matangazo ya tenders, electronic markets na faida nyingine za kiuchumi.

Imeandikwa na Dotto Kahindi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents