Habari

Snapchat waja na ‘Snap Map’ inayokuwezesha kufuatilia matukio kwa ramani (+Video)

Kampuni ya Snap Inc kupitia App yake ya snapchat leo imeongeza Feature mpya inayoitwa Snap Map, sehemu hiyo ambayo itakusaidia kujua nini kinatokea popote ulipo kwa kutumia ramani maalumu iliyoko kwenye programu hiyo imezinduliwa rasmi siku ya jana na sasa inapatikana kwenye programu za mifumo yote ya Android pamoja na iOS.

Tokeo la picha la snap map

Akielezea jinsi inavyofanya kazi ‘Snap Map’ kupitia mtandao wa Refinery29, Mtengenezaji wa bidhaa wa kampuni ya Snap Inc, Jack Brody amesema unapo update programu ya snapchat utapelekwa kwenye hatua chache ambazo zitakuwa zikikuelekeza jinsi ya kuingia kwenye Snap Map na baada ya hapo utatakiwa kuwasha sehemu maalum ya location ili uweze kutumia sehemu hiyo kisha utaweza kuchagua ulipo alafu moja kwa moja utaruhusu mahali ulipo kuonekana na marafiki baadhi au marafiki wako wote hiyo inategemeana na wewe kisha hapo utakuwa uko tayari kutumia sehemu hiyo mpya ya snap map.

https://youtu.be/bvl82FfnUvw

Akiendelea kuielezea sehemu hiyo ya Snap Map inavyofanya kazi, Jack Brody amesema kwa kutumia snap map unaweza kujua kinachoendelea kwa marafiki zako lakini pia unaweza kujua nini kinachotokea kwa kutumia sehemu hiyo, kwa kutumia sehemu hiyo snap map inauwezo wa kuonyesha sehemu yenye tamasha au mkusanyiko wa watu wengi kwa kutumia “map heat” hii ikionyesha watu wengi wanaotumia snapchat walipo kwa pamoja hivyo kukupa urahisi wa kujua mahali penye matamasha na mikusanyiko ya watu ambayo pengine ni muhimu kwako.

Sehemu hiyo mpya kwa sasa tayari inapatikana kwenye programu zote za snapchat unaweza ku-update ili kupata sehemu hiyo na kuanza kushiriki na marafiki zako kujua sehemu za bata popote ulipo, Kama huna programu hiyo ya snapchat basi ni wakati wa kudownload sasa ili uweze kuona matukio live yanayotokea kwenye viwanja vya bata iwe usiku au mchana.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents