Fahamu

Mtandao wa WhatsApp waeleza namna ya kuficha mawasiliano yako yasidukuliwe

Mtandao wa WhatsApp waeleza namna ya kuficha mawasiliano yako yasidukuliwe

Taarifa kwamba “WhatsApp inaweza kudukuliwa” sio jambo ambalo mtumiaji yoyote wa mtandao huo wa kijamii anataka kusikia wala kuona katika kichwa cha habari. Alafu kuongezea kwamba “Wadukuzi walifanikiwa kuweka mfumo wa uangalizi” na kitengo cha habari cha kampuni hiyo wana kibarua kikubwa mikononi mwao.

WhatsApp inasema akaunti kadhaa zililengwa na ” mdukuzi mkuu wa mitandao”. Lakini iwapo kauli hii imekutia wasiwasi, haya ni baadhi ya mambo unayostahili kufanya kuhakikisha mawasiliano yako yapo salama.

cyber attack

Kwa mujibu wa BBC. Udukuzi huo uligunduliwa kwanza mapema mwezi huu. Wakati huo Facebook, inayomiliki mtandao wa WhatsApp, iliwaambia maafisa wa usalama kwamba lilikuwa : “pengo katika mawasiliano ya sauti ya WhatsApp VOIP [voice over internet protocol] iliyoruhusu udukuzi kupitia vifurushi vya mfumo wa SRTCP [secure real-time transport protocol] vilivyotumwa kwa nambari ya simu ya mlengwa.” Hebu tulifasiri hilo – ina maana wadukuzi walitumia simu ya WhatsApp kupiga kwa nambari ya mlengwa.

Hata kama simu haikushikwa, mfumo huo wa udukuzi uliidhinishwa kutokana na pengo hilo katika mawasiliano ya sauti ambao hauna usalama wa kutosha. Simu pengine ilikatika na haionekani kwenye orodha ya waliopiga simu katika simu yenyewe, kwasababu wadukuzi walikuwa tayari wameidhibiti.

messaging logoskwasababu mara nyingi huwa umeimarisha kinga kwa simu yako Hapana, sio kwamba ukiizima simu na kuiwasha utakuwa umetatua tatizo. Siku ya Jumatatu , WhatsApp ilependekeza wateja bilioni 1.5 waimarishe programmu hiyo tumishi baada ya kusambaza mfumo huo mpya ulionuiwa kulinda vifaa vinavyotumia mtandao huo dhidi ya udukuzi. Licha ya kwamba WhatsApp inalinda mawasiliano ya wateja wake, inayomaanisha kwamba ujumbe unaonekana upande wa anayeupokea pekee, mfumo huo wa udukuzi ungemruhusu mshambuliaji aweze kuusoma ujumbe huo. Kwa hivyo ni vyema uimarishe ‘updates’ – kwasababu mara nyingi huwa umeimarisha kinga kwa simu yako.
cyber attackHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Licha ya kwamba mawasiliano yanalindwa katika WhatsApp, epuka kuhifadhi taarifa zako kwenye anga la mtandao kama Google Drive au iCloud, hapo kuna tatizo. Anga hilo la mtandao halina usalama kwahivyo mtu yoyote anaweza kuingia na kuyafikia mawaslinao yako yote. Iwapo unajali faragha, basi hilo ni jambo ambalo unapaswa kufikiria kuacha kulifanya. Huenda ukapata ujumbe kwamba hifadhi mawasiliano yako – lakini iwapo unataka kulibadili hilo hivi sasa nenda kwenye eneo la kuhifadhi chati zako yaani Chat Backup, katika eneo la mpangilio wa simu yako – settings.

cyber attackHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Kuna programu saidizi za kuimarisha ulinzi, uthibitisho wa mara mbili (2FA) kabla kuingia kwenye mtandao huo ambao ni njia nzuri ya kuweka data yako salama. Ni kama wingu la ziada la usalama kuhakikisha watu wanaojaribu kuingia katika akaunti ya mtandao ni watu asili wanaosemakuwa ni wao. Kwanza, mteja ataingiza jina lake na nywila. Baada ya hapo watahitajika kutoa alama za vidole, au sauti yao au nambari maalum zitakazotumwa na programu hiyo kwenye simu yako ambazo utatumia kufungua na kuingia kwenye akaunti ya Whatsapp na nyinginezo za kijamii. Unaweza kulibadili hilo pia kwenye upande wa mpangilio wako wa simu. Udukuzi huu huenda ni jambo la dharura iwapo wewe ni wakili, mwanaharakati, au mwandishi habari. Kwa mujibu wa kamati ya kuwalinda waandishi habari, huenda hawa ndio watu ambao wamelengwa katika udukuzi huu.

By Ally Juma.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents