Habari

Mtandao wa WhatsApp waleta sintofahamu India, Watumiaji waagizwa kupakua App nyingine

Mtandao wa WhatsApp waleta sintofahamu India, Watumiaji waagizwa kupakua App nyingine

Shirika kuu la usalama wa mtandao nchini India, Cert, imewaomba watumiaji wa mtandao wa WhatsApp kupakua programu mpya ( ya hivi punde) katika simu zao baada ya kugundua kuwa kulikuwa na programu mpya ya udukuzi katika programu ya awali ya ujumbe wa programu hiyo.

Programu hiyo ya software ilisababshwa na faili ya video iliyotumwa kutoka kwa namba isiyojulikana.

Katika taarifa , WhatsApp ilisema kuwa haikuwa na sababu ya kuamini kuwa watumiaji wa simu waliathiriwa.

Taarifa ya programu hiyo ya udukuzi ilikuja muda mfupi baada ya WhatsApp kukiri kuwa programu yake ilitumiwa katika kuweka mfumo wa ujasusi kwenye simu.

Facebook ambayo inamiliki mtandao wa WhatsApp, ilikuwa imetangaza kuwepo kwa udhaifu wa usalama wa mfumo wa WhatsApp siku chache zilizopita.

Ilisema kuwa watumiaji wanapofungua faili zao za video, programu hiyo ya software inajiweka yenyewe katika simu- katika mtindo sawa na ule wa udukuzi wa programu inayofahamika kama Pegasus, unaoaminiwa kuwa umekuwa ukitumiwa dhidi ya waandishi wa habari na wanaharakati.

Cert imesema kuwa programu hiyo iliruhusu washambulia wa kimtandao kuingilia simu na kufanya mabadiliko katika kifaa, bila kujadi simu iko sehemu gani kijiografia.

Programu hiyo ya udukuzi inahitaji tu mtumiaji wake kufungua faili ya video, kinyume na ile ya Pegasus ambayo kusababisha athari pale mpokeaji wa simu kupitia WhtatsApp anapoijibu.

Programu ya ujumbe imesema pia kwamba ilikuwa imetoa maagizo mapya ya usalama ya hivi punde ambayo yanaweza kuzuwia udukuzi huo.

India ina watumiaji wa mtandao wa WhatsApp milioni 400, idai inayoifanya nchi hiyo kuwa yenye soko kubwa zaidi la mtandao huo dunia.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents