Michezo

Mtangazaji maarufu wa radio nchini Rwanda aacha kazi kisa Messi na Argentina

Mwandishi wa Habari za michezo na Mtangazaji maarufu wa radio nchini Rwanda, Rutamu Elie Joe amejikuta akiacha kazi yake hiyo baada ya kuahidi kuwa angeacha kazi hiyo endapo Messi na timu yake ya Argentina ingetolewa kwenye michuano ya kombe la dunia.

Image result for Rutamu Elie Joe
Rutamu Elie Joe

Rutamu amesema kuwa amechukua maamuzi hayo baada ya kutoa kauli iliyonukuliwa akisema ”Messi asipochukua Kombe la Dunia basi mimi naachana na hii kazi yangu ya utangazaji wa mpira pamoja na kufanya kazi katika kituo hiki cha redio” kauli hiyo aliitoa akiwa hewani kwenye kituo cha Radio 1 cha nchini Rwanda wakati wa mechi ya ufunguzi kati ya Urusi na Saudia Arabia.

Kwa mujibu wa gazeti la The New Times Rwanda limeeleza kuwa mtangazaji huyo kwa sasa ameacha kazi na hakuamini kama watu walichukua kauli yake kwa umakini.

Nilikuwa nafikiria ni kauli ya kawaida tu kama kipindi cha kawaida ambacho kimepita kumbe watu walinirekodi na wakasalia kimya kimya na nikaanza kuona wananiandama mitandaoni.“ameeleza Rutamu.

Kwenye mahojiano yake aliyofanya na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), Rutamu amesema kuwa alianza kuona video na sauti yake aliyoahidi kuacha kazi ikisambaakwa kasi mitandaoni baada ya mchezo wa kwanza wa Argentina dhidi ya Iceland kumalizika kwa sare ya goli 1-1 .

Mechi za Kombe la Dunia, mechi ya kwanza Iceland ilitoka droo na Argentina ndio nikaanza kuona sasa zile kanda zikianza kusambaa mitandaoni kila mahali na hapo ndipo watu walianza kuuliza kwamba nilisema Messi atakuwa mshindi kwenye Kombe la Dunia sasa wanatazamia ahadi yangu itimie.”Rutamu ameiambia BBC.

Argentina imetolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia Jumamosi ya wikiendi iliyopita kwa kipigo cha goli 4-3 dhidi ya Ufaransa.

Kwa mujibu wa habari kutoka gazeti la The New Times Rwanda, Rutamu kwa sasa anatarajia kuacha kazi rasmi Julai 15, 2018 siku ya fainali ya Kombe la Dunia na ameeleza kuwa atafanya kazi nyingine ili kutimiza ahadi yake kwa wasikilizaji wake.

Rutamu alishawahi kuwa msemaji mkuu wa klabu ya Sunrise ya nchini Rwanda kabla ya kujiingiza kwenye masuala ya uandishi wa habari na utangazaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents