Burudani

Mtangazaji maarufu wa TV nchini Uingereza, atumia kiswahili kumjibu shabiki yake mtandaoni

Mtangazaji maarufu zaidi nchini Uingereza, Piers Morgan ametumia kiswahili kupokea pongezi kutoka kwa shabiki yake aliyevutiwa na utangazaji wake.

Image result for piers morgan
Piers Morgan

Morgan ambaye anatangaza kipindi pendwa nchini Uingereza cha Good Morning Britain kinachorushwa na ITV, amemshukuru shabiki huyo kwa kumwambia ‘Asante Sana’.

Hata hivyo, baadhi ya watu waliotoa maoni juu ya Tweet hiyo ya kiswahili wanaonekana kutoelewa lugha hiyo na wamekuwa wakiuliza maana yake.

Piers Morgan mwenye wafuasi zaidi ya milioni 6 kwenye mtandao wa Twitter, Tweet yake ya kiswahili inatosha kushawishi watu wengine waanze kufuatilia au kujifunza zaidi kiswahili.

Tayari nchi kadhaa ikiwemo Afrika Kusini, imeshatangaza lugha ya kiswahili kuanza kutumika kwenye mitaala ya Elimu ya Msingi ifikapo mwaka 2020.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents