Tragedy

Mtangazaji mkongwe Julius Nyaisangah afariki dunia kwa ugonjwa wa Kisukari

Mtangazaji mkongwe nchini Julius Nyaisangah maarufu kama Uncle J, amefariki dunia leo Alfajiri kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.

424976_333927119973228_1272853026_n

Nyaisangah alikuwa Meneja wa kituo cha radio cha Abood FM pamoja na Abood TV cha mjini Morogoro.

409553_343315309034409_1871709246_n
Julius Nyaisangah wa mbele akiwa na aliyekuwa mtangazaji mwenzie wa Radio One, Charles Hilary

Akiongea kwa simu na Bongo5, Kaimu Meneja wa Abood FM, Abeid Dogoli ambaye pia ni Afisa Masoko wa kituo hicho, amesema marehemu Nyaisangah ameacha mke na watoto watatu.

“Kaenda hospitali jana mchana saa nane na amefariki leo Alfajiri lakini kabla ya hapo alikuwa akienda hospitali kupata matibabu na kuweza kurudi,” amesema Dogoli. “Mipango ya mazishi tunasubiri ndugu walioko Dar es Salaam, walioko Tarime ili wakae kama familia wapange msiba utakuwa wapi.”

422893_343314539034486_1145949422_n
Watangazaji wa zamani wa Radio One, akiwemo Nyaisangah

Akimuongelea, Nyaisangah aliyewahi pia kuwa mtangazaji wa Radio One, Dogoli amesema Nyaisangah hakuwa tu meneja wa kituo hicho cha radio, bali alikuwa kama mwalimu wa watangazaji na pengo lake haliwezi kuzibika.

“Alikuwa na mtu wa msaada mkubwa kama unavyomfahamu ni mtu unique, ana vitu ambavyo wengine hawana na aliweza kuwabadilisha wafanyakazi wa Abood Media na wakafika sasa kuwa katika hali ya ubora. Kifo chake kimetuhuzunisha sana, kila mtu ameguswa na pengo lake litachukua muda kuweza kupata mtu kuliziba. Kupata mtu wa aina yake itachukua muda.”

Mungu ailize roho yake mahala pema poponi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents