MichezoTragedy

Mtangazaji wa michezo wa East Africa Radio Kenneth Kidago afariki dunia

Mbunifu Msaidizi na Mtangazaji wa Habari za Michezo wa East Africa Radio Kenneth Kidago Lyanga amefariki dunia nyumbani kwake Mwenge Mlalakua, Jijini Dar es Salaam.

942154_599744393390797_682502294_n

Mipango ya mazishi ya Kenneth Lyanga inafanywa na familia yake.

Kabla ya kujiunga na East Africa Radio, Ken alikuwa mkuu wa vipindi wa kituo cha radio cha Best FM cha wilayani Ludewa na kabla ya hapo aliwahi kuwa mtangazaji wa Triple A FM ya Arusha.

Profesa Jay ameandika: Nimepokea kwa masikitiko na mshtuko mkubwa sana taarifa za kifo cha rafiki yangu KEN KIDAGO. ..Hadi mauti yanamkuta alikuwa ni mfanyakazi wa EA RADIO/ EATV… Lakini hapo mwanzo alishawahi kufanya kazi Radio Ukweli (Moro) na Triple A few. Poleni wote ndugu, jamaa, na marafiki, Tulimpenda ila Mwenyezi Mungu Amempenda zaidi, jina lake LIHIMIDIWE na Ampumzishe BROTHER K mahali pema PEPONI. …AMEN!

Naye Afande Sele ameandika:

Wkt huo kituo cha radio(fm) moro kilikuwa kimoja tu nacho ni Ukweli fm kinachomilikiwa na kanisa katoliki jimbo la morogoro,kisanii nilikuwa mchanga sana nikifanya kaz chini ya kaka,rafiki na mwlmu wangu jose mbilinyi(Sugu),CD zilikuwa ni kitu adimu na chenye thamani sana kiasi kwamba nyimbo nilizokuwa nashirikishwa na sugu ktk albam zake nyingi hazikuwa zinapelekwa radioni kama’single’zilikuwa zinabaki ndani ya albam tu(kanda za casset) ili kusukuma mauzo kwa mashabiki,lkn kulikuwa na dj/mtangazaji mmoja tu ndani ya radio ukweli nyakat hizo aliyekuwa ananikubali sana kama msanii wa kwanza kutoka moro kwenda dar ‘kibishi’ na kufanya kazi bora kabisa nikiwa na msanii mkubwa na mkali aliyekuwa anatisha kwa nyakat zile 2 proud,mr 2 baadae sugu na leo ni mh sugu,huyu dj/mtangazaj alikuwa na kiu kubwa ya kuona mimi nasikika kwa mashabiki wa nyumbani moro kwa kila hali hivyo akawa anathubutu kucheza hewani pale redioni zile nyimbo nilizoshirikishwa na sugu kwa kutumia’Tape’kanda za kaseti’kilazima’ na kweli watu walisikia nami nikasikika ikawa ndio mwanzo wa mimi kukubalika nyumbani na ugenini,yeye aliitwa keneth kidago lyanga maarufu kama brother’K’,baadae alihamia triple A fm Arusha,nj na mwisho alikuwa est africa radio akitumikia vipind vya michezo zaid,nina taarifa za kuumiza sana moyo wangu juu ya mtu huyu,Keny????RiP ndg wa damu!,,,,
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents