Habari

Mtanzania akamatwa Indonesia akiwa na dawa za kulevya kilo 1 tumboni (Picha)

Raia mmoja wa Tanzania aliyetambulika kwa jina la Abdul Rahman Asman anadaiwa kukamatwa Bali nchini Indonesia akiwa na dawa za kulevya alizokuwa amemeza tumboni.

Maofisa katika Uwanja wa Ndege wa Bali wameliambia Shirika la Habari la AFP kuwa Mtanzania huyo alikamatwa Januari 30, 2019.

Wamesema alipopekuliwa alibainika alikuwa amemeza dawa hizo ambazo hata hivyo hazikufafanuliwa ni za aina gani. Lakini baadhi ya ripoti zilisema dawa alizokutwa nazo zinafahamika kwa jina la methamphetamine.

“Mtanzania huyo alikamatwa Bali akiwa na kilo kadhaa za dawa hizo,” chanzo cha habari kilisema.

Taarifa zaidi zimedai kuwa alipofanyiwa uchunguzi wa XRay na CT scan aligundulika kuwa na paketi kadhaa za plastiki na ndani yake kukiwa na unga.

Haikulezwa ni lini atapandishwa mahakamani na haikufahamika mara moja iwapo upande wa mashtaka utataka mtuhumiwa huyo ahukumiwe adhabu ya kifo. Indonesia inatajwa kuwa ni moja ya mataifa duniani yenye sheria kali dhidi ya makosa yanayohusiana na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Kuna mlolongo wa watuhumiwa wanaosubiria adhabu ya kifo wakiwamo raia wa Uingereza, Marekani na wengine kutoka Afrika Magharibi ambao wamenyongwa ahadi kufa baada ya kutiwa hatiani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents