Mtanzania amwanika Obama

Image
Leo ikiwa ni mwaka mmoja kamili tangu Rais Barack Obama achukue Ikulu ya Marekani, Mwandishi Mtanzania ambaye amekaa ughaibuni kwa zaidi ya miaka 30, Julie Majuva, amezindua kitabu chakeĀ  ‘Barack Obama: The African-American president’ ambacho kinaelezea undani wa sera za Rais huyo na jinsi alivyofanikiwa kuleta mapinduzi kwenye siasa ya taifa hilo kubwa kabisa duniani kiasi cha kutunukiwa tuzo ya Nobel

Akielezea zaidi, Julie amesema kuwa kitabu hicho ambacho tayari kimeshauzwa zaidi ya nakala 254 000 Ulaya kimewalenga zaidi vijana ambao wanafikiri maisha mazuri yako mbele kwa mbele na kusahau kwamba mabadiliko huanzia nyumbani.

Kitabu hicho kitakuwa mitaani wiki chache zijazo na kitatafsiriwa katika lugha ya nyumbani mwishoni mwa mwaka huu

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents