Michezo

Mtanzania apoteza pambano la Ubingwa, Mrusi aomba marudiano 

Bondia wa kike kutoka Dar es Salaam Tanzania, Sarafina Julias Bela amejikutaka akipoteza katika pambano lake la raundi 10 mbele ya Mrusi Anna Levina.

Sarafina Julias aliingia ulingoni majira ya saa tatu usiku jijini Moscow kumkabili, Anna Levina katika kugombea mkanda wa ubingwa wa Dunia wa IBA ( International Boxing Association) na WPBF ( World professional Boxing Federatin) kwa upande wa wanawake.

Bela alijikuta akipoteza pambano hilo la uzito wa Lightweight (Kg 48) kwa pointi baada ya kumalizika bili kushudiwa mtu akidondoshwa.

Hata hivyo bondia huyo Mtanzania alicheza vizuri raundi zote 10 na kuonekana kulimudu vema pambano hilo licha ya kushindwa kummaliza mpinzani wake kwa Knockout na matokeo yake kuufanya mchezo kwisha kwa kuwaachia majaji watatu kutoa maamuzi.

Licha ya kupoteza, promota wa Kirusi, Mr Shamo ameomba marudiano (rematch) baada ya kuvutiwa nanamna Mtanzania huyo alivyokuwa akipigana.

https://www.instagram.com/p/B6F0EeshLsx/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents