Michezo

Mtanzania ‘Rose Seif’ awanyoosha Wakenya kwenye riadha

Mwanariadha Rose Seif, ameweka rekodi mpya katika mashindano ya Afrika ya Mashariki na Kati ‘Kanda ya Tano’ ya riadha kwa vijana baada ya kuibuka na medali mbili za dhahabu.

Mtanzania ainyoosha Kenya, aweka rekodi Afrika
Rose Seif

Rose ameshinda medali hizo katika mbio za mita 400 na mchezo wa mruko wa chini (long jump) kwenye fainali zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wikiendi iliyopita.

Mara baada ya ushindi huo Rose amesema ushindi huo umetokana na nidhamu, usikivu na maandalizi kwani ndiyo chachu ya ushindi kwa mwanamichezo anaehitaji kufikia malengo yake.

Namshukuru Mungu kwa matokeo haya, si jambo rahisi lakini kipindi hiki nimefanya vizuri kutokana na maandalizi tuliyopewa na walimu wetu hakuna kinachoshindikana duniani ukiwa na nidhamu na kujituma“,Alisema Rose Seif kwenye mahojiano yake na Bongo Five.

Rose alitwaa medali ya dhahabu ya mruko wa chini akiruka umbali wa mita 5.16 na medali ya mita 400 akikimbia kwa sekunde 60:95.

Matokeo hayo ya Rose yanafanya Tanzania kuibuka na medali sita za dhahabu za mbio hizo zilizofungwa jana jioni na Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Muhammed Kiganja.

Mzanzibar Daud Dahasheghe aliibuka kinara katika mchezo wa kurusha mkuki, akirusha umbali wa mita 49 na sentimita 68.

Mashindano hayo yalishirikisha nchi saba ambazo ni Tanzania,Sudan ya Kusini, Eritrea, Kenya, Somali, Sudan pamoja na Zanzibar inayoingia kama nchi kamili. 

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents