Habari

Mti waua familia Arusha

Watu wa tano wa familia moja wamefariki baada ya nyumba waliokuwa wakiishi kuangukia na mti katika kijiji cha Gilesi, wilaya ya Arumeru mkoani Arusha kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani humo Charles Mkumbo “Kifusi hicho ambacho kiliambatana na huo mti, kilishuka hadi sehemu ya bonde ambapo kulikuwa na nyumba ya Bwana huyu Jonathan na kuifunika hiyo nyumba na kusababisha familia yake kufariki dunia,” alisema kamanda Charles Mkumbo

Mwenyekiti wa kijiji cha Gilesi, Amoni Elami alisema wananchi walijitolea kuondoa mabaki ya mti huo pamoja na kujenga nyumba ya dharula ili familia hiyo iweze kusitirika.

“Tutafanya kila iwezekanalo kujenga nyumba ya dharula ili baba huyu na mama huyu, ili wananchi wapate mahali pa kuwafikia, tunaomba kwa ruhusa ya mkurugenzi ile miti iliyobaki turuhusiwe kuondoa ili isije ikaleta maafa mengine kama haya.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents