Michezo

Mtibwa Sugar yadhihirisha ubora wake Inno Uefa League

Kikosi cha vijana cha Mtibwa Sugar hapo jana kimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Inno Uefa League hii ikiwa ni katika harakati za kuendelea kuwa na timu imara.

Katika mchezo wa kundi A wa michuano hiyo, kikosi hicho cha vijana kiliweza kumaliza mchezo wake wa mwisho kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mauzo, lililofungwa na Nassoro Ally (Chollo).

Kikosi cha wana tam tam kimeweza kushinda michezo yake yote mitano katika hatua hiyo na kufanikisha kukusanya pointi 15, kikiwa katika kundi moja na timu za Lusaga, Black Star (Njia Panda), Mauzo, Volcan na , White Star.

Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya vijana, Edwin Hagai kupitia mtandao wa timu hiyo amesema dhumuni lao ni kutwaa ubingwa wa Inno Uefa League.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents