Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Mtibwa Sugar yamnasa kinda aliyecheza michuano ya Gabon

Klabu ya Mtibwa Sugar wamefanikisha kuongeza kandarasi ya Nickson Clement Kibabage  kuendelea kutumikia kikosi hicho cha wana tam tam.

Mkataba wa beki huyo wa pembeni  ulikuwa unaelekea mwishoni na viongozi wa wana tam tam wakiongozwa na mkurugenzi  mtendaji  wa klabu Jamal Bayser wamefikia makubaliano ya kumuongeza Kibabage kandarasi ya miaka miwili kabla ya mkataba wa awali kumalizika.

Kibabage amesaini kandarasi ya kuendelea kutumikia kikosi  katika ofisi ndogo zilizopo jijini Dar es laam chini  ya Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo, Jamal Bayser

Nickson Kibabage anayemudu kucheza beki wa pembeni na kiungo mshambuliaji amekuwa katika kiwango bora msimu uliomalizika katika mashindano ya vijana pia katika ngazi ya timu ya taifa ikiwemo kuwakilisha taifa katika mashindano ya CAF nchini Gabon.

Kibabage amejiunga na klabu ya Mtibwa Sugar kupitia cha kukuza vipaji cha Mtibwa Sugar Academy (under 20) na kabla ya hapo alikuwa anachezea Moro Kids.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW