DStv Inogilee!

Mtibwa Sugar yatangaza kikosi dhidi Nothern Dynamo michuano ya CAF Confederation Cup 

Klabu ya Mtibwa Sugar ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Afrika ( CAF Confederation Cup ), leo siku ya Jumanne wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Nothern Dynamo ya Usheli Sheli katika mchezo huo utakao pigwa viunga vya Azam Complex wa Chamazi, Mbagala majira ya saa 10:00 jioni, tarehe 27.11.2018.

Akizungumza na waandishi wa habari kocha wa Mtibwa, Zubery Katwila amesema ni lazima anahakikisha wanapata ushindi na huwenda akatumia washambuliaji wawili ili kupata matokeo wakiwa nyumbani.

”Siifahamu kwa undani Northern Dynamo lakini tumepewa udhaifu wao na ubora wao, kwenye ligi yao siyo wabaya wanacheza vizuri na wanapata matokeo,” amesema Katwila.

“Kama imepata nafasi ya kushiriki mashindano haya inamaanisha imefanya vizuri kwao, tutakuwa makini na ubora wao ili kufanya vizuri kwenye mchezo wa kwanza.”

Wachezaji saba waliokuwa katika timu ya taifa ya vijana Ngoro Ngoro worriors wakiwemo, Kelvin Sabato, Salum Kihimbwa, Ismail Aidan, Dickson Job, Kibwana Ally Shomary, Nickson Kibabage na Abuutwalib Mshery wapo na timu hiyo kwa sasa kwaajili ya kuivaa Nothern Dynamo.

Kikosi cha Mtibwa Sugar kitakachoshuka uwanjani leo

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW