Makala

Mtibwa v Kagera “classical match”

Wafalme wa soka kutoka mji kasoro bahari Morogoro Mtibwa Sugar wanataraji kushuka dimabani November, 19 katika mchezo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League)   dhidi ya Kagera Sugar.

Mtanange huo namba 70 wa Vodacom Premier League  unatarajiwa kuwa wa kipekee mbali na baadhi za Sukari ambazo hutolewa klabu hizi mambo yanayoufanya mchezo huu kuwa wa kipekee “Classic match” ni haya hapa,

Ushindani wa kibiashara

Mtibwa Sugar na Kagera Sugar ni timu mbili zinazomilikiwa na viwanda vya kuzalisha sukari hapa nchini kutokana na timu hizi mbili kuzalisha bidhaa moja na hii inaongeza chachu ya ushindani uwanjani.

Katwila V Mexime

Makocha hawa wawili wa vilabu viwili wamecheza wote katika klabu ya wana tam tam Zuber Katwila “Puchetino” akiongoza akiwa idara ya kiungo huku Mecky Mexime akiongoza idara ya ulinzi, baada ya wote kucheza kwa pamoja kwa muda mrefu na kugeukia fani ya ukocha na wote walitumikia benchi la ufundi la wana tam tam, Mexime alikuwa kocha mkuu huku Katwila akiwa msaidizi wake.

Maisha ya Mexime katika mpira yalianzia Mtibwa Sugar na mwaka jana alijiunga na Kagera Sugar na baada ya kuondoka Mtibwa Sugar Mecky Mexime amekutana na Zuberi Katwila “Puchetino” katika michezo miwili ya ligi kuu bara na kila mmoja akishinda mchezo mmoja mmoja.

Makocha hawa vijana waliotengenezwa katika viungo vya Manungu Arena watakuwa chachu ya mchezo huu kuwa mchezo wa kipekee hivyo ni moja ya vivutio katika mchezo namba 70 wa ligi kuu bara.

Kagera Sugar haijawahi kushinda Manungu

Zaidi ya misimu saba ya Ligi kuu bara (Vodacom Premier League) Mtibwa Sugar hawajawahi poteza mchezo wowote mbele ya Kagera Sugar katika uwanja wake wa nyumbani Manungu. Katika misimu hiyo saba timu timu hizi zimekutana mara 7 na wana tam tam wamefanikiwa kushinda michezo mitano na sare mbili.

Katika michezo hiyo 7 ya ligi kuu bara wana tam tam wamefanikiwa kufunga magoli tisa  katika michezo hiyo huku Kagera Sugari wakifunga magoli matatu.

Mecky Mexime, Jaffary na Ozuka  warejea nyumbani

Mecky Mexime, Jaffary Salum Kibaya na  Ozuka Izechuku  ni baadhi ya nyota walioibuliwa na Mtibwa Sugar na kukulia katika viunga vya Manungu na sasa wako katika timu ya Kagera Sugar.

Mexime anarejea akiwa kama kocha wa kikosi hicho huku Jaffary atarejea kama mchezaji wa Kagera Sugar na amewahi kutumikia kikosi cha Mtibwa Sugar na alikulia katika timu ya vijana na baadaye akapandishwa katika timu ya wakubwa na kwa upande wa Ozuka alikuwa katika katika timu ya vijana ya Mtibwa Sugar kabla ya kwenda Azam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents