Tragedy

Mtoto afa kwa kuripuliwa

MTOTO mwingine mwenye umri wa miaka mitano, Sheila Simon ameuawa kwa kuchomwa moto unaodaiwa kulipuliwa kwa mafuta ya taa na watu wasoijulikana kwa kile kinachohusishwa na ulipizaji kisasi.

Na Daniel Mjema, Moshi

 

 

 

MTOTO mwingine mwenye umri wa miaka mitano, Sheila Simon ameuawa kwa kuchomwa moto unaodaiwa kulipuliwa kwa mafuta ya taa na watu wasoijulikana kwa kile kinachohusishwa na ulipizaji kisasi.

 

 

 

Tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita majira ya saa 5:00 usiku katika eneo la Msaranga.

 

 

 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng�hoboko, jana alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusisitiza kuwa, hayuko tayari kuzungumzia zaidi tukio hilo kwa sababua likuwa nje ya ofisi.

 

 

 

� Ninachoweza kusema kwa sasa ni kuthibitisha tu kwamba tukio hilo lipo lakini taarifa zaidi nitawapeni kesho kwa sababu sina details (taarifa) za tukio hilo siko ofisini kwa sasa, ” alisema Ng�hoboko.

 

 

 

Habari zaidi zimedokeza kuwa, mapema kabla ya tukio hilo, mtu anayedaiwa kuhusika na mauaji hayo, alifika katika nyumba hiyo na kuwaondoa watoto wengine waliokuwa wakiishi na baba yao.

 

 

 

Inadaiwa kuwa, kabla ya kutokea kwa tukio hilo, kulikuwa na taarifa za vitisho vilivyokuwa vikitolewa na mtu huyo dhidi ya baba wa watoto hapo katika Kituo cha Polisi cha Majengo Mjini Moshi.

 

 

 

Inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio baba wa watoto hao na mkewe walikwenda kupata kinywaji katika baa moja na kumwacha aliyeuawa akiwa amelala ndani.

 

 

 

Habari hizo zimedai kuwa mtu au watu wasiojulikana walifika katika nyumba hiyo na kumwagia mafuta ya taa katika mito ya samani na kuiwaisha na moto wake kuteketeza vitu kadhaa vya ndani na kumuua mtoto huyo.

 

 

 

Inaendelea kudai kuwa, muuaji wa mtoto huyo alitumia namba ya simu iliyofichwa kuwaarifu ndugu mahali ulipo mwili huo wake.

 

 

 

Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents