Bongo5 Exclusives

Mtoto aliyezaliwa na virusi vya Ukimwi apona nchini Marekani

Wanasayansi wametangaza kuwa mtoto aliyekuwa amezaliwa na virusi vinavyosababisha Ukimwi amepona na hana tena virusi hivyo.

research_635x250_1362347326

Mtoto huyo wa huko Mississippi nchini Marekani amekuwa akitumia dawa kwa mwaka sasa na haoneshi kuwa na maambukizi hayo tena. Hata hivyo hakuna uhakika asilimia 100 kuwa mtoto huyo amepona kabisa lakini vipimo vya hali ya juu vimetuka kumpima na haoneshi kuwa na virusi tena.

Habari hii inaweza kuwa mwanzo wa kupatikana tiba ya ugonjwa huo unaosababisha vifo vya watu wengi hususan barani Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents