Burudani

Mtoto wa Diamond, Tiffah anyemelea anga za Asahd wa Dj Khaled

Hakuna ubishi kuwa mtoto wa Diamond Platnumz, Tiffah ni maarufu zaidi katika ile orodha ya watoto wa mastaa Bongo.

Sio Bongo pekee, Diamond anamtaja Tiffah kama miongoni mwa watoto wanaofuatiliwa zaidi katika mitandao ya kijamii; My Miss World….. Most Followed Female kid in the WORLD!!!’

Ndiyo, ni kweli Tiffa anafuatiliwa zaidi kwenye mitandao, ukurasa wake wa Instagram una followers Milioni 1.8. Ikiwa ni tofauti ya followers 100,000 na mtoto wa Dj Khaled, Asahd mwenye followers Milioni 1.9.

Hivyo Diamond anapoeleza kuwa mwanae ni miongoni mwa watoto wa kike wanaofuatili zaidi duniani (Most followed female kid in the world) anamaanisha.

Tiffah ambaye alizaliwa August 6, 2015 alifikisha followers Milioni 1 katika mtandao Instagram November 30, 2016.

Watoto wengine wa mastaa Bongo wenye followers zaidi ya 100,000 ni Jaden wa Ray Kigosi na Chuchu Hansy, followers 171k na Cookie wa Aunt Ezekiel na Mose Iyobo, followers 420k

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents