Michezo

Mtoto wa Didier Drogba apata shavu ligi kuu ya Ufaransa

Klabu ya soka ya En Avant de Guingamp ambayo inashiriki ligi kuu ya Ufaransa, imetangaza kumsajili mchezaji Isaac Drogba (17) amabye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba.

Isaac amewahi kucheza katika chuo cha soka cha Chelsea nchini Uingereza.

Kupitia mtandao wa Instagram, Drogba ameonyesha kufurahishwa na hatua hiyo kubwa aliyopiga mwanae kwa kuandika, “Couldn’t be more proud of you @isaacdrogba11 @eaguingamp Fiers de toi @isaacdrogba11 @eaguingamp.”

Frank Lampard ambaye amewahi kucheza na Drogba katika timu ya Chelsea, kupitia mtandao huo ame-comment kwa kuandika, “Congratulations! I remember Isaac as the small polite boy! Now a man!.”

Naye John Terry hakutaka hilo limpite akaamua ku-comment kwa kuandika, “Can’t believe how big he is mate, congratulations.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents