Michezo

Mtoto wa George Weah aipeleka Marekani kombe la dunia

Mtoto wa aliyekuwa mchezaji nguli wa mpira wa miguu duniani, Timothy Weah ameisaidia timu ya taifa ya Marekani kukata tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia kwa vijana waliyo na umri chini ya miaka 17.

Timothy Weah ambaye ni mtoto wa mchezaji bora miaka ya 1995, George Weah ameifungia bao katika mchezo huo ambao waliibuka na ushindi wa 6-2 dhidi ya Cuba mjini Panama.

Weah anaekipiga katika kikosi cha vijana cha PSG ameifungia timu ya taifa ya Marekani bao lake la pili katika mashindano hayo dakika ya 88.

Marekani itaingia tena Uwanjani siku ya Jumapili kuvaana na timu ya Mexico au Costa Rica.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents