Michezo

Mtoto wa gwiji wa soka Brazil, Pele afungwa jela miaka 33

Mtoto wa gwiji wa soka Brazil na duniani kote, Pele, Edinho Pele, amefungwa jela miaka 33 kwa kufanya biashara haramu ya pesa au kujipatia pesa chafu zilizotokana na biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya. Edinho ni mchezaji soka mstaafu, aliyecheza kama mlinda lango katika klabu ya Santon aliyowahi kuchezea Pele mapema miaka ya tisini.

edinho_pele

Alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 na kutumikia kifungo kwa kosa la ulanguzi wa dawa za kulevya pamoja na kuwa na uhusiano na mlanguzi sugu wa dawa hizo mjini Santos. Edinhio, alikiri kosa la kuwa mraibu wa dawa za kulevya lakini alikanusha madai ya kuhusika na ulanguzi wa dawa hizo.

Uamuzi wa mahakama ulitolewa mjini Praia Grande, katika jimbo la Sao Paulo. Vyombo vya habari nchini humo bado havijaweza kupata kunena na Edinho, ambaye jina lake halisi ni Edson Cholbi do Nascimento, lakini vinasema kuwa huenda akakata rufaa.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents