Burudani

Mtoto wa Kanye West na Kim Kardashian ‘North West’ kutambulishwa rasmi kwa dunia mwezi (July) kupitia kipindi kipya cha TV cha mama mkwe wa Kanye ‘KRIS’

Familia ya mkali wa ‘Yeezus’ Kanye West na Kim Kardashian imegoma kabisa kuweka hadharani picha za mtoto wao ‘North West’ kwa sasa, na Kanye hana mpango wa kumtumia mwanae kupata pesa wala kuboost shughuli zake za muziki. Lakini wawili hao wanategemea kumwonesha hadharani mtoto huyo kupitia kipindi kipya cha TV mwezi ujao (July).

kim n kanye

Kanye na Kim wameamua kutokutoa picha za mwanao na badala yake fans wategemee kumwona live North West kupitia TV talk show mpya ya mama yake na Kim aitwaye Kris Jenner (mama mkwe wa Kanye) ambayo inategemewa kuzinduliwa mwezi ujao (July 15) siku ambayo ndio North atatambulishwa rasmi kwa dunia kupitia kipindi hicho.

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa Hollywood Life exclusively kuwa sababu ya wazazi hao kuruhusu kumtambulisha mwanao North katika show hiyo, ni kutokana na kwamba Kris ni familia hivyo wameamua vitu vyote kuhusu North vianzie katika familia.

Vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa na kiu ya kupata picha za mtoto huyo hata kwa gharama yoyote, kitu ambacho hakijamshawishi baba mtoto Kanye ambaye hataki kumfanyia biashara mwanae mpenzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents