Habari

Mtoto wa kiume wa Ghadafi, Saif al-Islam ahukumiwa kifo

Mahakama nchini Libya imemhukumu mtoto wa kiume wa Col Muammar Gaddafi, Saif al-Islam, na wengine wanane adhabu ya kifo kutokana na makosa ya kivita yanayotokana na mapinduzi ya mwaka 2011.

0EE7611E00000578-3177048-image-a-8_1438074733100

Saif al-Islam hakuwepo mahakamani japo alitoa ushahidi kupitia link ya video.

Anashikiliwa na kundi la waasi wa zamani katika mji wa Zintan ambao wamekataa kumkabidhi kwa serikali. Wengine waliohukumiwa kifo ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa ujasusi katika uongozi wa Gaddafi, Abdullah al-Senussi pamoja na waziri wa zamani, Baghdadi al-Mahmoudi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents