Habari

Mtoto wa miaka 10 aruhusiwa kutoa mimba

Madaktari wamekubali ombi la msichana wa umri wa miaka 10, ambaye ni muathiriwa wa ubakaji kutoka jimbo la Haryana kaskazni mwa India la kutoa mimba.

Dk Ashok Chauhan aliiambia BBC kuwa hatua hiyo sasa inaweza kuchukuliwa wakati wowote. Msichana huyo alipata ujauzito karibu miezi mitano iliyopita baada ya kubakwa na baba wa kambo ambaye hata hivyo amekamatwa.

Sheria nchini India haziruhusu utoaji mimba baada ya wiki 20, bila ya idhini ya madaktari kwa kuwa huweka maisha ya mwanamke hatarini.

Uamuzi wa kumruhusu msichana huyo kutoa mimba ulichukuliwa baada ya mahakama kuwaambia madaktari kuwa itakubali.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents