Habari

Mtoto wa miaka 15 mbaroni kwa kudanganya kutekwa nyara na kuomba hela ya kukombolewa kwa baba yake

Mtoto wa miaka 15 mbaroni kwa kudanganya kutekwa nyara na kuomba hela ya kukombolewa

Polisi katika mji wa Jos nchini Nigeria wanachunguza ni jinsi gani mvulana mwenye umri wa miaka 15 alivyodanganya kuwa ametekwa nyara na kuomba kikombozi kutoka kwa baba yake ili aachiliwe. ” Ni tukio lililofanyika kwa utalaamu ,” msemaji wa polisi Terna Tyopev alisema.

Kijana huyo na marafiki zake wengine wanne wanaomzidi umri, ambao kwa sasa wamekamatwa na kuwekwa mahabusu ,walidai kikombozi cha naira 500,000 sawa na dola 1,365 , amesema

Walikuwa wamepanga kutumia pesa hizo kwa ajili ya sherehe za mahali ya kumaliza shule.

Siku tatu kabla ya kupanga utekeji nyara huo feki , bada yake na mvulana huyo alikuwa ameuza gari lake kwa ajili ya matumizi ya kifamilia.

Mvulana huyo mwenye umri wa miaka 15 alipanga mpango huo baada ya kuisaka familia yake na kubaini kuwa pesa alizopata baba yake baada ya kuuza gari zilikuwepo.

“Pesa zilikuwa zimelipwa kwenye akaunti ya benki ya baba yake , kwa hiyo hazikuwepo ,” Amesema Bwana Tyopev.

Mvulana alipanga utekaji nyara huo wa bandia baada ya kufahamu kuwa baba yake alikuwa ameuza gani na alikuwa na pesaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMvulana alipanga utekaji nyara huo wa bandia baada ya kufahamu kuwa baba yake alikuwa ameuza gani na alikuwa na pesa

Marafiki zake walijifanya kuwa watekaji nyara wake na kuwasiliana na baba yake.

“Walimuonya kuwa mtoto wake amepelekwa mbali na Jos na kwamba hapaswi kuripoti kwa maafisa wowote wa usalama . Baba yake alifuata muongozo wao na aliripoti tu pale alipoona mambo yamekuwa hatari sana ,” amesema msemaji wa polisi.

Utekaji nyara huo uliingia dosari pale maafisa walipofuatilia nambari ya simu iliyotumiwa kuomba kikombozi katika makazi mjini Jos.

Mvulana huyo na marafiki zake walikuwa wanafanya mazungumzo wakati polisi walipovamia jengo walimokuwemo

“Baba yake alihisi vibaya sana wakati ilipogundulika kuwa alikuwa ni mtoto wake. Mtoto wake alikuwa hajamuomba pesa ya sherehe ,” Bwana Tyopev alisema.

Mkuu wa polisi Mohammed Adamu (pichani) alisema kati ya miezi ya Januari na Aprili mwaka huu takriban watu 685 kote nchini Nigeria
Image captionMkuu wa polisi Mohammed Adamu (pichani) alisema kati ya miezi ya Januari na Aprili mwaka huu takriban watu 685 kote nchini Nigeria

Ingawa mpango ulikuwa ni wa mtoto wake, utekelezaji wa mpango huo uliokuwa wa kitaalamu ulifanywa na marafiki zake waliokuwa na umri wa miaka kati ya 18 na 22 – jambo lililowafanya maafisa kuwashuku.

Kwa mujibu wa BBC. Polisi kwa sasa wanachunguza ikiwa vijana hao walishawahi kuwatekeji nyara w watu wengine kwa lengo la kudai kikombozi awali , anasema Tyopev.

Utekeji nyara unaolenga kudai kikombozi umekithiri ni nchini Nigeria . Magenge ya watekaji nyara huwateka tajiri na maskini kote nchini humo , na mara kwa mara watekani wamekuwa wakikusanya hadi dola 150,000 -na wakati mwingine huwauwa wanaotekwa ambao familia zao zinashindwa kulipa kikombozi.

Mkuu wa polisi Mohammed Adamu alisema kati ya miezi ya Januari na Aprili mwaka huu takriban watu 685 walitekwa nyara kutoka maeneo mbalimbali nchini Nigeria.

By Ally juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents