Habari

Mtoto wa Michael Jackson, Paris ahamishiwa katika hospitali ambayo baba yake alikatia roho

Jumamosi (June 8) mtoto wa kike wa hayati Michael Jackson aitwaye Paris Jackson alihamishiwa katika hospitali ya UCLA Medical Center ambapo ndipo alilazwa MJ June 25, 2009 na mauti kumkuta.

paris-2

Paris mwenye miaka 15 alifikishwa katika hospitali ya Los Angeles Jumatano (June 5) alikolazwa kwa saa 72 kabla ya kuhamishiwa UCLA Medical Center baada ya jaribio lake la kujiua kugonga mwamba.

Kwa mujibu wa chanzo kati ya sababu ambazo zinahisiwa kusababisha maamuzi magumu aliyoyachukua Paris kutaka kujiua ni pamoja na matatizo ya kifamilia ambayo yamekuwepo kwa kipindi kirefu toka MJ afariki dunia mwaka 2009.

Mtandao wa TMZ umefanikiwa kupata video ya tukio zima wakati Paris anaingizwa hospitalini hapo, itazame hapo chini

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents