Habari

Mtoto wa muuza madawa ya kulevya sugu duniani El Chapo, aachiwa huru baada ya mapigano kutokea – Video

Mtoto wa muuza madawa ya kulevya sugu duniani El Chapo, aachiwa huru baada ya mapigano kutokea - Video

Siku ya Alhamisi usiku Jeshi la Polisi nchini Mexico liliamua kumuachia huru mtoto wa kiongozi wa kundi la dawa za kulevya kwenye mji wa Sinaloa baada ya kuzidiwa uwezo na vikosi vya kundi hilo.

Ovidio Guzmán (28) ambaye ni mtoto wa muuza dawa za kulevya maarufu duniani El Chapo aliachiwa huru baada ya mapigano makali yaliyohusisha silaha za moto kwenye mji wa Culiacán nchini Mexico.

Wizara ya ulinzi nchini humo ikiongozwa na Waziri Alfonso Durazo imesema walifikia maamuzi ya kumuachia masaa machache baada ya kumkamata ili kuweza kunusuru wananchi mitaani waliokuwa hatarini kutokana na mapigano hayo.

Kukamatwa kwake kunakuja mwezi mmoja baada ya baba yake Joaquín “El Chapo” Guzmán kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kwa usambazaji wa dawa za kulevya na uhalifu.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents