Michezo

Mtoto wa Phil Neville afuata nyayo za baba yake

Mtoto wa mchezaji wa zamani wa Manchester United, Phil Neville anayejulikana kwa jina la Harvey amefuata nyayo za baba yake baada ya kuingia kandarasi na mashetani hao wekundu.

Neville Snr mwenye umri wa miaka 16 ameutambulisha ulimwengu wa soka kuwa amesajiliwa na United baada ya kuposti picha yake kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram hapo jana siku ya Jumanne akiandika kuwa anafuraha mara mbili moja kusajiliwa na ya pili ikiwa ni siku yake ya kuzaliwa.

Phil ambaye kwa sasa ni meneja wa timu ya taifa ya Uingereza kwa upande wa wanawake wanawake ameiwakilisha klabu hiyo ya Old Trafford mara 386 wakati wa miaka 15 akiwa na United. kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram amemtakia mwanae, Harvey Neville mafanikio mema katiki kipindi hiki ambacho anakwenda kutimiza ndoto zake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents