Habari

Mtoto wa Prince William aanza shule

Mjukuu kutoka familia ya Kifalme nchini Uingereza Prince George, hatimaye ameanza elimu yake ya awali siku ya jana(Alhamis).

Prince George alisindikizwa na baba yake Prince William katika shule binafsi ya Thomas’s Battersea, iliyopo karibu na kasri ya Kensington.


Mtoto huyo wa kwanza wa Prince William alivalia mavazi nadhifu na yakupendeza huku akionekana mwenye adabu na busara kwa Mkuu wa Shule hiyo baada ya kupokelewa.

Mama yake Kate, hakuoneka eneo hilo yeye alibakia nyumbani kwa ajili ya kujipumzisha kutokana na ujauzito aliyonao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents