Soka saa 24!

Mtoto wa Sergio Aguero afuata nyayo za baba yake kwa hili

Mtoto wa nyota wa Manchester City, Sergio Aguero anayejulikana kama, Benjamin ameamua kufuata nyayo za baba yake baada ya kuamua kutia dawa nywele zake ambazo zinamuonyesha katika muonekano mpya na wa tofauti.

Ilikuwa kabla ya kipindi cha Christmas ambapo straika huyo wa Argentina, aliungana na wachezaji wenzake kama Robert Lewandowski na Lionel Messi katika muonekano huo mpya wa nywele kwakuzitia dawa.

Benjamin mwenye umri wa miaka tisa, amefuata nyayo za baba yake kwa kuzitia dawa nywele zake siku ya Alhamisi mchana.

Mara baada ya kutengeneza muonekano huo mpya, Benjamin alimpigia baba yake kupitia ‘video-called’ akimtaka kurejea nyumbani kwao Argentina ili kumuonyesha.

Kufuatia simu hiyo, Aguero aliamua kuposti kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo ali ‘screenshot’ na kujilinganisha na mtoto wake katika aina hiyo ya nywele.

Aguero anaonekana kuzidi kuwa kwenye kiwango kizuri ndani ya City, wakati timu yake ikiwa mwenyeji siku ya Jumapili mchana kwenye mchezo dhidi ya Chelsea.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, ametupia ‘hat-trick’ kwenye mechi iliyomalizika 3 – 0 dhidi ya Arsenal Jumapili iliyopita kaba kuisaidia timu yake mbele ya Everton kwenye dimba la Goodison Park siku ya Jumatano.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW