Habari

Mtoto wa Whitney Houston asemekana kupokea tuzo ya Mama yake akiwa amevuta!

Mtoto wa marehemu Whitney Houston, ameamsha hisia tofauti kati ya mashabiki wa muziki, hasa wa marehemu mama yake baada ya kusadikika kwamba alivuta bangi kabla ya kupokea tuzo kwa niaba ya Mama yake Whitney Houston katika tuzo za Billboard Music Awards za nchini Marekani.

Katika show iliyofana zaidi ya kawaida, wanamuziki John Legend na Jordin Sparks waliimba nyimbo za marehemu Whitney Houston kwa ajili ya kutambua mchango wake kimuziki na kuenzi uhai wake. Marehemu alipewa tuzo ya Lifetime Achievement ambayo ilipokelewa na mtoto wake, ambamo ndimo watu walihisi, kutokana na tabia yake Bobbi Christina, kwamba yawezekana hayuko sawa na ametumia kitu.

Baada ya show, mtoto huyo wa Whitney alitoka nje na kunaswa kwenye picha na rapper Wiz Khalifa huku habari zikitanda kwamba alikua anashiriki kuvuta bangi na kupelekea kudhibitisha yale yaliyokua yakisemwa na watu.

Wanafamilia ya Houston wamesema wataliingilia swala hili na kuhakikisha kama ni kweli, Bobbi anapata msaada anaohitaji. Hii sio mara ya kwanza msichana huyo anasemekana kutumia madawa kwani ripoti zinasema baada ya kumzika mama yake, alipotea ambapo alienda kutumia na baadaye kurudi.

Habari hizi zinasikitisha kwani kilichomuua mama yake dada huyu ni matumizi hayo ya madawa na ingawa inasemekana Bobbi hajabobea bado, inapasa familia iingilie kati haraka na mapema iwezekanavyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents