Burudani

Mtu anayeweza kutumia twitter amepevuka – Madee

Msanii wa Bongo Flava, Madee ameeleza jinsi anavyotumia mtandao wa twitter na kubainisha wanaoweza kutumia mtandao huo ni wale waliopevuka.

Madee amesema twitter ni sehemu ambayo anaiheshimu kuliko mtandao wowote kwa sababu ni tofauti na facebook  na instagram.

“Mtu ambaye anaweza kutumia twitter ni mtu ambaye amepevuka kwa sababu kule kuna watu wa aina nyingine kabisa, hakuna matusi kama tunavyoona instagram na facebook, hakuna kuchambana kule ni kuelimishana,” Madee ameiambia Bongo5.

Ameongeza kuwa, “yeyote ambaye hajawahi kutumia twitter akianza ataenjoy kinoma, ndio maana nikiandika kitu chochote kule twitter lazima kiwe kikubwa, kwa sababu watua wanaokiona na wanaokisoma ni wenye hekima na akili,” amesema Madee.

Madee katika mtandao wa twitter anafollowers 30.5k na instagram followers milioni moja.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents