Habari

Mtu mmoja akamatwa kwa tukio la kigaidi Uingereza

Ikiwa ni siku chache tangu kutokea moto mkubwa na kusababisha vifo vya watu kadhaa katika jengo la Grenfell Tower, bado taifa hilo la Uingereza limezidi kuandamwa na majanga.

Inaelezwa kuwa mwanamume mmoja amekamatwa na polisi kwa kuhusishwa na shambuluo linalohusishwa na ugaidi na kupelekea kifo cha mtu mmoja na wengine wanne kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari karibu na msikiti mmoja uliopo kaskazini mwa nchi hiyo.

Mtu huyo aliyekuwa na gari aligonga umati wa watu waliokuwa wakitembea kwa miguu, Nalo Baraza Kuu la Waislamu nchini humo limeleza kuwa tukio hilo liliwalenga waumini wake waliokuwa wamemaliza swala ya jioni katika msikiti huo.

Hili ni tukio la tatu mfululizo kwa nchi hiyo kwa mwaka huu kwa ni tukio la kwanza lilokuwa la kigaidi lilitokea Mei 23 katika tamasha la mwanamuziki Ariana Grande na kusababisha vifo kadhaa na majeruhi, huku tukio la pili ni lile la kuungua moto jengo la ghorofa 24 liitwalo Grenfell Tower na kusababisha vifo vya watu 79 kwa mujibu wa mtandao wa Daily  Mail na hili ni la tatu.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents