Habari

Mtu mmoja anusurika kifo baada ya kudondokea juu ya gari kutoka ghorofa ya 14

Hakika kama siku yako haijafika basi hata upate ajali ya aina gani utatoka mzima, kama ilivyomtokea mtu mmoja huko Ureno, baada ya kudondoka kutoka ghorofa ya 14 na kuangukia juu ya paa la gari iliyokuwa imeegeshwa chini ya jengo hilo.

ajali-1

Kwa mujibu wa The Sun Kama picha inavyojionesha, mtu huyo mwenye miaka 28 alidondokea juu ya gari hiyo aina ya Honda Civic ambayo katika picha inaonekana imeharibika kwa juu na kubaki na alama za damu.

Ajali-2

Wakazi wa eneo hilo katika mji wa Quarteira huko Ureno wanadai walisikia kishindo kikubwa mida ya saa saba mchana na katika hali ya kushangaza walimkuta mtu huyo eneo la tukio akiwa mzima na anazungumza.

Mtu huyo alipelekwa hospitali na polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents