Habari

Mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani aliye hai ‘World’s oldest person’ agundulika Afrika Kusini (picha)

Mtu anayeaminika kuwa na umri mkubwa zaidi duniani amegundulika katika mji mdogo wa kusini-magharibi ya Johannesburg, Afrika Kusini anakoishi.

bibi-2

Yawezekana wapo wengine kusikojulikana lakini bibi Johanna Mazibuko mwenye miaka 119 ndiye anayeaminika kuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani, kwa mujibu wa BBC.

Bibi Mazibuko aliyezaliwa mwaka (1894) kwa mujibu wa vyeti vyake ameivunja rekodi ya ‘Guiness World Records’ ambayo inamtaja Misao Okawa kutoka Japan kuwa ndiye mwenye umri mkubwa aliye hai kwa kuwa na miaka 115.

bibi-1
Bibi Mazibuko akiwa na mwanae mwenye miaka 77

Hata hivyo mtu mwenye umri mkubwa zaidi aliyewahi kuwekwa katika rekodi za dunia alikuwa Jeanne Calment kutoka Ufaransa aliyefariki August 4, 1997 akiwa na miaka 122.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents