Tragedy

Mtu wa tano afa

Mtu mwingine ameripotiwa kufa kwa homa ya bonde la ufa, wilayani Monduli mkoani hapa, siku tisa baada ya harusi yake.

Na Adam Ihucha, Arusha
Mtu mwingine ameripotiwa kufa kwa homa ya bonde la ufa, wilayani Monduli mkoani hapa, siku tisa baada ya harusi yake.

Kifo hicho kinafanya idadi ya watu waliokufa kutokana na ugonjwa huo toka uripotiwe kuwepo nchini kufikia watano.

 

Siku tatu zilizopita, mtu wa nne aliripotiwa kufa wilayani Tarime mkoani Mara, huku akiwa na dalili nyingi za ugonjwa huo.

Idadi hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizopo kwenye vyombo vya habari.

Ofisa Afya mkoa wa Arusha, Bw. Crispin Shayo, alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kumtaja mtu aliyefariki kuwa ni Bw. Kisioki Kipong`i.

Hata hivyo, alisema taarifa kamili ya kifo hicho anaisubiri kutoka kwa maofisa wenzake kutoka wilayani Monduli.

`Taarifa niliyonayo ni ya mdomo tu kuwa mtu mmoja anasadikiwa kufa kwa kupata virusi vya ugonjwa huo,` alisema.

Alisema mtu huyo ambaye alitoka kufunga ndoa siku tisa zilizopita, anatoka katika kabila la Kimasai katika kijiji cha Losimingori, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20.

Kwa mujibu jamaa zake waliohudhuria msiba wake kijijini hapo, mazishi hayo yalifanyika chini ya uangalizi maalumu wa maofisa wa afya.

`Mmoja wa ng`ombe wake alikufa kwa ugonjwa unaosaidikiwa kuwa ni bonde la ufa (Rift Valley), siku mbili kabla ya kifo cha kijana huyo,` alisema.

Kwa mujibu wa ndugu wa kijana huyo, baada ya ng�ombe huyo kufa kijana huyo alimchuna ngozi na kula nyama yake na alianza kujisikia vibaya baada ya kula nyama hiyo.

Walidai kuwa alifikiri ana malaria na kuanza kutumia dawa za kutibu malaria lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya na kukimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Monduli, ambapo baada ya siku sita alikufa.

Ugonjwa huo huwapata wanyama na binadamu huambukizwa virusi hivyo kwa kula nyama ama kuumwa na mbu walionyanya damu ya wanyama waliokuwa na virusi hivyo au kunywa maziwa yasiyochemshwa au vitu vya majimaji kutoka kwa wanyama hao.

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents